Majeneza ya Ali Khamenei na wanafamilia wake wanne yakiwa ndani ya sanduku la kioo

Chanzo cha picha, HAMSHAHRI

Iliyochapishwa

Muda wa kusoma: Dakika 6

Ibada ya mazishi ya Ali Khamenei iliyoanza Ijumaa iliyopita na itakamiliko leo kwa maziko yake katika kaburi la Imam Reza mjini Mashhad.

Majeneza ya kiongozi wa zamani wa Iran na jamaa zake wanne yaliwekwa hadharani katika eneo maalum jijini Tehran asubuhi ya Jumamosi, Julai 4, 2026. Majeneza hayo yaliyokuwa yamefunikwa kwa bendera ya Iran, yalikuwa marefu zaidi kuliko majeneza ya kawaida, na yaliwekwa ndani ya vizimba vya vioo.

Mbali na masuala ya kiusalama, majeneza hayo yalikuwa ndani ya kizimba cha vioo kuashiria matumizi ya mfumo wa kudhibiti wa halijoto.

Hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu majeraha yaliyosababisha kifo cha Ali Khamenei;kichosemwa na maafisa ni kuhusu ukubwa wa milipuko.

Baada ya kutangazwa kwa kifo cha Kiongozi Mkuu wa Iran na kucheleweshwa kwa mazishi yake, maswali mengi yaliibuka katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu utaratibu wa mazishi hayo na sheria za Kiislamu zinasema nini kuhusu suala hilo. Kujibu maswali hayo maafisa wa Iran walitoa ufafanuzi chache kabla ya mazishi yake.

Iman Attarzadeh, msemaji wa kamati ya maandalizi ya mazishi, alisema: “Mwili umehifadhiwa kwa heshima na uangalifu mkubwa, kwa kuzingatia kanuni za kidini na kisheria, na haukuzikwa wala kuwekwa mahali fulani kama amana.”

Iman Attarzadeh hakufafanua zaidi jinsi ya “kuzingatia viwango vya Sharia,” lakini aliangazia zaidi mazishi ya muda miongoni mwa Waislamu inayoitwa “wadieh.”

Pengo la muda kati ya mauaji ya Ali Khamenei na kuzikwa kwake limezusha swali la “vigezo vya Shariah” kwa Muislamu aliyefariki na kuna hukumu gani kwa mazingira haya?

Jeneza la Ali Khamenei lilifunikwa kwa bendera ya Iran, lilionekana kuwa refu zaidi kuliko majeneza ya kawaida, na liliwekwa ndani ya kizimba cha vioo.

Chanzo cha picha, ISNA

Umuhimu wa “kulinda heshima ya maiti” katika Uislamu

Kuanzia wakati ambapo roho inapotoka mwilini mwa mwanadamu yeyote, mwili wa marehemu huchukuliwa kuwa wenye kuheshimika, na utaratibu wa kidini huzingatiwa hadi wakati wa mazishi. Desturi hii wakati mwingine hutokana na hadithi na simulizi, na wakati mwingine hutokana na mapokeo na utamaduni.

Uislamu una mtazamo maalum kuhusu “utakatifu” wa maiti. Dini hii inazingatia mazishi ya haraka kuwa sehemu ya utakatifu huo.

Wakati wa mauaji ya kikatili yaliyotokea Januari mwaka jana—ambapo miili ya waandamanaji ilirundikwa kwenye makontena na malori, na picha zenye kuhuzunisha za jinsi miili hiyo ilivyoshughulikiwa zilichapishwa—mjadala uliibuka kuhusu sababu za kutozingatiwa kwa heshima ya marehemu na familia zao zenye majonzi, kinyume na msisitizo na kanuni za Kiislamu, huku vikwazo na masharti ya kiusalama yakiwekwa katika mazishi yao.

Hassan Fereshtian, mtafiti wa masuala ya dini, alisema katika mahojiano na BBC Persian(Kifarsi): “Katika sheria za Kiislamu (fiqh) za madhehebu ya Shia, maiti ya hupewa heshima sawa na ymtu mwenyewe akiwa hai. Kwa sababu hiyo, kuna kanuni za kulinda utakatifu hata wa miili ya maadui.”

Kulingana na yeye, katika zama za kabla ya Uislamu na katika baadhi ya vita vya kikabila, ilikuwa desturi kuharibu vibaya mwili wa adui baada ya kumuua, na kukata viungo vya mwili huo kulichukuliwa kuwa ishara ya ushindi. Uislamu ulipinga hili na kulichukulia hatua hiyo kuwa haramu. Kuashiria kuwa, hata adui aliyeuawa ana hadhi takatifu na hapaswi kudhalilishwa au kuvunjiwa heshima.

Kwa mujibu wa mtafiti huyo, kuna sababu kama tatu hivi za kulinda heshima ya marehemu. Kwanza, marehemu ana familia na jamaa wanaomjali, na kudhalilisha maiti huumiza hisia zao. Pili, kulinda heshima ya marehemu ni sehemu ya maadili ya jumla ya jamii, na kutokuheshimu mwili wa mwanadamu kunaweza kudhoofisha thamani hiyo ya kijamii. Tatu, hata alama na vitu vilivyobaki vya mtu huheshimiwa na wale walio hai.

Pia anabainisha kuwa sheria za Kiislamu zina hukumu maalum kuhusu vitendo vya kuufanyia ukatili mwili wa marehemu. Kama vile kumdhuru mtu aliye hai kunavyoambatana na hukumu na wajibu wa kidini, kuna kanuni maalum pia kuhusu kukata viungo au kuufanyia ukatili mwili wa maiti; jambo linaloonyesha kuwa mtu anaendelea kuwa na hadhi takatifu hata baada ya kufariki dunia.

Mwaka jana, mjadala wa maadili ya Kiislamu uliibuka kuhusu sababu ya kutozingatiwa kwa heshima ya marehemu na familia zilizofiwa, kwa kuzingatia msisitizo na misingi ya Kiislamu.

Uislamu na kuharakisha mazishi

Katika mafundisho ya Kishia (Imamiyya), kuna msisitizo mkubwa wa kuharakisha mazishi. Wanazuoni wa Kishia wamesema kuwa mwili wa marehemu haupaswi kuwekwa bila sababu, na mazishi yanapaswa kufanyika haraka iwezekanavyo kama kuna dharura au sababu muhimu.

Hassan Fereshtian, mtafiti wa masuala ya dini, anaelezea umuhimu wa kuharakisha mazishi katika mafundisho ya madhehebu ya Waislamu wa Kishia na Sunni akisema: “Kuharakisha mazishi ni moja ya mambo yanayopendekezwa na kusisitizwa na Sharia, lakini katika mafundisho ya Kishia, jambo hili si wajibu wa kidini, sharti la kidini, wala wajibu wa kisheria (wa lazima).”

Kwa mujibu wa Bw. Fereshtian, mapendekezo mengi katika maandiko ya dini yana lengo la kutoa mwongozo; yaani, pamoja na kipengele cha kidini, yanashughulikia pia masuala ya kijamii na kiafya. Wakati ambapo hakukuwa na vifaa vya kuhifadhia maiti, kuchelewesha mazishi kungeweza kusababisha matatizo ya kiafya, na hivyo msisitizo uliwekwa katika kuharakisha mazishi.

Anaeleza kuwa katika mafundisho ya Kishia, ingawa kuharakisha mazishi kunapendekezwa, pendekezo hilo si la lazima. Sehemu ya msisitizo huu pia inatokana na heshima kwa marehemu pamoja na hadhi yake katika jamii. Hata hivyo pendekezo hili huchukuliwa kwa uzito zaidi miongoni mwa Wasunni, na baadhi ya wanazuoni wanaamini kuwa, ikiwezekana, marehemu azikwe siku hiyo hiyo na kabla ya kuzama kwa jua.

Hassan Fereshtian anaongeza kuwa katika miongo ya hivi karibuni, uchunguzi wa kitaalamu wa maiti (forensics), taratibu za kiutawala, na mipango ya familia kwa ajili ya shughuli za maombolezo imesababisha muda kati ya kifo na mazishi kwa kawaida kuwa zaidi ya siku moja.

“Mazishi ya uaminifu” ni nini?


Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Hezbollah nchini Lebanon, aliuawa tarehe 25 Septemba 2024, na mazishi yake yalifanyika tarehe 25 Februari 2025, miezi mitano baadaye.

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati habari za kuzikwa kwa Ali Khamenei kwa namna ya “amana” na uaminifu katika mji wa Qom zilipokataliwa, swali liliibuliwa: ni ubora gani na wingi wa mazishi ya aina hii?

Aktolea mfano dhana ya “kuaminiana,” Hassan Fereshtian anasema kwamba katika desturi ya Washia, kuna aina nyingine ya maziko ambayo haichukuliwi kuwa kaburi la kudumu. Kwa kuzingatia hili, mwili wa marehemu ulizikwa mahali kwa muda hadi ulipohamishwa hadi eneo linalohitajika kwa wakati ufaao.

Anabainisha kuwa nchini Iran, hasa kuanzia zama za Qajar hadi sehemu kubwa ya zama za Pahlavi, familia za kidini wakati mwingine zilizika kwa muda miili ya jamaa zao ili kuihamishia Najaf au Karbala kwa wakati ufaao. Katika baadhi ya matukio, hata baada ya miaka, mifupa ya marehemu ilitolewa kutoka eneo la muda na kuhamishiwa kwenye kaburi la milele.

Kulingana naye, mfano unaojulikana sana ni kuzikwa kwa muda kwa Ali Shariati huko Zainabiyah, Syria. Pia kuna nyakati ambapo watu huzikwa kwa uaminifu kwa ajili ya uhamisho wa mahali pa wasia wa marehemu au mahali ambapo ni chaguo la familia.

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *