Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Othman Masoud Othman amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuunga mkono hatua ya maridhiano ya kisiasa kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na ACT-Wazalendo.
Othman amesema msimamo na uongozi wa Rais Samia katika kuunga mkono mchakato huo ni kauli nzito ya kiuongozi na alama muhimu ya hekima inayoonesha umuhimu wa hatua hiyo pamoja na mustakabali wa Zanzibar.
“Kwa upekee, nikushukuru kwa dhati Rais Samia, kuwepo kwako katika hafla hii ni kauli nzito ya kiuongozi na alama muhimu ya hekima na ni muongozo juu ya umuhimu wa jambo hili, ni kielelezo cha ulivyobariki hatua hii katika hatua zote na utakavyoendelea kutoa uongozi katika mchakato huu,” amesema.
(Feed generated with FetchRSS)