
Nchini Zambia wakati huu raia wakijiandaa kwa uchaguzi Mkuu wa mwezi ujao, Rais Hakainde Hichilema licha ya kupewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo kwa muhula mwengine, anatarajiwa kupimwa kutokana na rekodi yake ya mabadiliko ya kiuchumi aliyofanya tangu aingie madarakani, mpinzani wake mkubwa akiwa ni kiongozi wa upizani Brian Mundubile.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kuelekea uchaguzi huo, suala la uchumi linatajwa kuwa kigezo kikubwa kwa wagombea, Rais Hichilema akitarajiwa kupimwa kwa namna ameshugulikia changamoto za raia kiuchumi.
Alipoingia madarakani, nchi ilikuwa inakabiliwa na mzigo mkubwa wa madeni, serikali iliyopita ya marehemu Edgar Lungu, ikishindwa kuwalipa wakompeshaji wake na wakati mmoja kujitangaza mufilisi.
Licha ya kushugulikia madeni ya nchi kupitia mazungumzo ya wakopeshaji wa kimataifa, bado raia wa Zambia wanahisi gharama ya maisha ipo juu.
Upizani kwa upande wake unaonekana kutumia changamoto za uchumi kama silaha dhidi ya utawala wa Rais Hichilema kwenye kampeni zake.
Kando na changamoto ya uchumi, wapinzani wanamtuhumu Rais Hichilema kutia saini marekebisho ya katiba mwaka wa 2025, hatua inayoongeza idadi ya wabunge.
Katika hatua nyengine, Makamu wa Rais wa Zambia Mutale Nalumango, amenusurika kifo baada ya ndege yake kupata changamoto za kiufundi muda mfupi baada ya kuruka akiwa njiani kuelekea kwenye kampeni.