Wapinzani Kongo wapinga jitihada za Rais Tshisekedi za kuwania muhula wa tatu wa urais

Uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo utafanyika miaka miwili ijayo hata hivyo hali ya mivutano imepamba moto kati ya serikali na wapinzani tangu bunge la nchi hiyo lenye viti vingi vya wawakilishi kutoka chama tawala kupasisha pendekezo a kurefusha mihula ya rais kusalia madarakani.

Tshisekedi, mwenye umri wa miaka 63, amekuwa madarakani tangu mwaka 2019; na muhula wake wa pili na wa mwisho wa miaka mitano unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Hata hivyo hadi sasa bado hajaamua kuupasisha mswada huo kuwa sheria au la.  

Ukizungumza na waandishi wa habari jijini Kinshasa, muungano wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa jina la C64 umesema kuwa hautalegeza msimamo wake; na kuwataka wananchi kufanya “maandamano makubwa ya uhamasishaji tarehe 22 mwezi huu ili kushinikiza kujiuzulu Rais Felix Tshisekedi.”

Maandamano yalipaswa kufanyika Jumatano wiki hii, lakini muungano wa upinzani Kongo uliakhirisha tarehe hiyo baada ya Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi, ambaye ni kiongozi wa Umoja wa Afrika, kuwaalika kwa ajili ya mashauriano”.

Shirika la Haki za Binadamu la Human Rights Watch jana Alhamisi lililaani “matumizi ya nguvu kupita kiasi” ya askari usalama  wa Kongo dhidi ya waandamanaji, ikiwa ni pamoja na matumizi ya mabomu ya machozi na marungu kuwatawanya waandamanaji. “

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *