Iliyochapishwa

Muda wa kusoma: Dakika 2

Manchester United na Liverpool zimeanza mawasiliano ya kumwania Joao Gomes, Chelsea iko kwenye mazungumzo ya kumsajili Jonathan Rowe, huku klabu ya MLS ikipanga kufanya jaribio la kumsaka Mohamed Salah.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United na Liverpool zimeanza mawasiliano kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo wa Wolverhampton Wanderers na timu ya taifa ya Brazil, Joao Gomes, mwenye umri wa miaka 25, baada ya mpango wake wa kujiunga na Atletico Madrid kushindikana. (Globo – in Portuguese)

.

Chanzo cha picha, Rex Features

Wakati huohuo, Chelsea iko kwenye mazungumzo na wawakilishi wa winga wa Bologna, Jonathan Rowe, raia wa England mwenye umri wa miaka 23. Hatua hiyo inakuja huku ikielezwa kuwa winga wa Argentina, Alejandro Garnacho, mwenye miaka 22, anatarajiwa kuondoka klabuni. (Il Resto del Carlino – in Italian)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Klabu ya Sporting Kansas City inayoshiriki MLS inapanga kufanya jaribio kubwa la kumsajili mshambuliaji wa Misri, Mohamed Salah (34), kwa uhamisho wa bure baada ya kuondoka Liverpool. (Athletic)

Klabu kadhaa za England, zikiwemo Coventry City na West Ham United, zinafuatilia kwa karibu kiungo wa Bodo/Glimt, Patrick Berg (24), kufuatia kiwango chake kizuri cha uchezaji akiwa na timu ya taifa ya Norway kwenye Kombe la Dunia. (Teamtalk)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Everton inaonyesha nia ya kumsajili winga wa England wa Newcastle United, Jacob Murphy 31, ambaye amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake na klabu hiyo ya St James’ Park. (Talksport)

Real Madrid imepanga kufanya kikao na nyota wake wa Brazil, Vinicius Jr, kwa lengo la kukamilisha mazungumzo ya kuongeza mkataba wake, kufuatia taarifa zilizodai kuwa klabu hiyo ilikuwa ikifikiria kumuuza mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *