Katibu Mkuu wa Kataib Hizbullah nchini Iraq amesema kundi lake litaendeleza njia ya Muqawama na mapambano, akipuuza vitisho vya maadui na kuwataka maafisa wa serikali ya nchi hiyo na viongozi wa kisiasa kuheshimu matakwa ya taifa hilo la Kiarabu.

“Madhalimu wanapaswa kujua kwamba ni vigumu sana na hatuwezi kuvumilia kuona Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ambaye pia alikuwa kiongozi wa wapenda uhuru na mtetezi wa watu wanaokandamizwa duniani, akiuawa huku wauaji wake wakipuuza adhabu ya Mungu,” amesema Abu Hussein al-Hamidawi.

Ameongeza kwamba: “Shukrani kwa Mungu aliyetupa neema ya kufuata miongozo ya Ayatullah Khamenei kwa miongo kadhaa. Tutasimama imara katika njia yake, na kupata msukumo kutoka kwenye fikra zake.”

Al Hamidawi amesisitiza kwamba wenzake wamekuwepo kwa muda mrefu kwenye viwanja vya vita na wamekuwa wakishiriki katika mapambano mbalimbali na kuongeza kuwa, mapambano yao dhidi ya dhulma za utawala wa Baath ulioondolewa madarakani wa dikteta wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein, mapambano dhidi ya uvamizi wa muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani tangu walipoivamia Iraq mnamo Machi 2003, kufutilia mbali seli za kigaidi za makundi ya wanamgambo wa al-Qaeda na Daesh nchini Iraq na Syria, mashambulizi dhidi ya kambi za Marekani kote Asia Magharibi wakati wa Operesheni ya al-Aqsa iliyoongozwa na Hamas, pamoja na operesheni za kulipiza kisasi za Iran kwa vita vya uchokozi vya siku 12 vilivyoanzishwa na Marekani na Israel ni mifano muhimu ya ukweli huo.

Al Hamidawi pia ameapa kuendeleza uunga mkono wa dhati kwa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, na kumtii kikamilifu kiongozi wake mpya, Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei.

Mkuu wa harakati ya Kataib Hizbullah ya Iraq amesema kwamba ushiriki mkubwa wa Wairaqi katika kumuaga na mazishi ya Ayatullah Khamenei umethibitisha bila shaka kwamba wao ni taifa la Muqawama na Jihadi.

“Mahudhurio hayo muhimu yalikuwa kura ya maoni ya mamilioni ya watu na yenye maamuzi, ambapo Wairaqi wameojitolea kwa mara nyingine na kutangaza tena uungaji mkono na kushikamana kwao na Mhimili wa Muqawama na mapambano yake ya silaha,” Al Hamidawi amesema.

Serikali ya Iraq, kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, imethibitisha kwamba idadi ya washiriki katika mazishi ya Ayatullah Ali Khameni katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala ilikuwa watu milioni 10.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei na wanafamilia yake waliuawa shahidi katika shambulio la kigaidi mnamo Februari 28, lililofanywa na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya makazi ya kiongozi huyo mjini Tehran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *