Serikali imesema inaendelea kuonesha dhamira thabiti ya kuwekeza zaidi katika huduma za matibabu ya saratani katika mfumo wa fahamu (neuro-oncology), sambamba na kuimarisha mfumo wa afya nchini.

Akifungua Mkutano wa Kimataifa wa Wataalamu wa Saratani katika Mfumo wa Fahamu wa Nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SNOSSA), uliofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana, Dar es Salaam, Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Tanzania imeongeza uwezo wa uchunguzi, matibabu na upatikanaji wa vifaa tiba kuanzia ngazi ya huduma za msingi hadi Hospitali ya Taifa.

Aidha, amesema Serikali imepiga hatua kubwa katika huduma za matibabu ya saratani, ambapo kwa sasa hospitali tatu za kanda na hospitali tatu binafsi zimeanza kutoa tiba ya mionzi, zikikamilisha juhudi zilizokuwa zikiongozwa na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, ambayo imekuwa ikitoa huduma hiyo kwa zaidi ya miaka 30.

Mhariri | @rajjmsangi

#AzamTvUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *