Miezi miwili baada ya mlipuko wa virusi vya Ebola kuripotiwa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ugonjwa huo unaendelea kusambaa kwa kasi. Wizara ya afya nchini humo inasema, watu 754 wamepoteza maisha na kuna maambukizi zaidi ya 2,000 yaliyothibitishwa.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kutangazwa na janga hilo, Shirika la afya duniani, limeanza zoezi la kujaribu dawa zinazoaminiwa zinaweza kusaidia kumaliza ugonjwa huo huko Bunia.

Mlipuko huo wa Ebola  ulianzia mkoani Ituri, lakini sasa hivi umesambaa kwa kasi katika mikoa mingine kama Kivu Kivu Kaskazini, Haut-Uélé na Tshopo.

Wataalam wa afya wanaonya kuwa, maambukizi zaidi yanatarajiwa kushuhudia katika siku zijazo iwapo dawa au chanjo haitakuwa imepatikana.

Hospitali ya Rwampara nchini DRC .
Hospitali ya Rwampara nchini DRC . AFP – GLODY MURHABAZI

Kudhibiti maambukizi hayo, imekuwa kazi ngumu kwa sababu watu walioambukizwa wanaendelea kutembelea maeneo mbalimbali na kutatiza jitihada za kufuatilia waliopata ugonjwa huo.

Aidha, mgomo wa wahudumu wa afya katika maeneo yaliyoathirika, wanaodai kutolipwa marupurupu yao, pia kunatatiza jitihada za kushinda vita dhidi ya virusi vya Ebola aina ya Bundibugyo.

Ili kufanikiwa kushinda ugonjwa huu, watalaam wanasema ushirikiano wa uhakika unahitajika, ili kuzuia maambukizi zaidi na kuwazuia watu walioambukizwa kwenda katika maeneo ambayo yapo salama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *