
Mamlaka ya Ukraine imesema droni za kivita zilirushwa karibu na miji ya Dnipro na Kharkiv. Shabaha za droni hizo haikuwa wazi.
Shirika la habari la Ukrinform limeripoti kwamba mbali na droni hizo, ndege za kivita za Urusi pia zilitumika.
Mji wa Zaporizhzhya na vitongoji vyake pia vilishambuliwa kwa mabomu ya kuongozwa jana jioni.
Hakuna ripoti za majeruhi wala uharibifu
Hakukuwa na maelezo yoyote juu ya majeruhi au kiwango cha uharibifu uliosababishwa na mashambulizi hayo.
Ukraine inaaminika pia kurusha droni usiku kucha kuelekea Urusi.
Viwanja vya ndege vya Kaluga, Volgograd, na Saratov nchini Urusi vilisimamisha kwa muda shughuli za ndege bila kutoa sababu zozote maalum, kwa kawaida hatua hiyo ikionekana kuwa onyo la uwezekano wa mashambulizi ya droni .
Jeshi la Ukraine halijatoa tamko lolote kuhusu hali hiyo.