Wafanyakazi wa huduma za uokoaji kaskazini-magharibi mwa Nigeria jana waliendelea kuwatafuta manusura baada ya boti iliyokuwa imebeba watu kadhaa kupinduka na kuzama katika jimbo la Jigawa.

Msemaji wa polisi katika jimbo hilo, Shi’isu Adam, ameeleza kuwa watu wasiopungua 40 walizama majini wakati wakati walipokuwa wakivuta mto wakiwa ndani ya boti. Wanawake na watoto ni kati ya watu waliozama katika ajali hiyo ya boti.

Gavana wa jimbo la Jigawa kaskaizni magharibi mwa Nigeria amesema kuwa wafanyakazi wa huduma za uokoaji jana walifanikiwa kuitoa miili sita majini.

Shirika la Taifa la Kushughulikia Masuala ya Dharura na Majanga ya Kimaumbile  la Nigeria kwa upande wake limetoa takwimu tofauti na ya chini zaidi. Limeripoti kuwa vifo vitano vimethibitishwa kufikia sasa, huku watu wasiopungua 20 wakiwa bado hawajulikani walipo.

Limeongeza kuwa, abiria 15 waliokuwa katika boti hiyo wamenusurika kifo.

“Operesheni ya utafutaji na uokoaji bado inaendelea,na inaaminika kwamba boti hiyo ilikuwa imebeba watu wasiopungua 40,” amesema Nura Abdullahi, Msemaji wa shirika hilo katika jimbo la Jigawa.

Ajali za boti ni jambo la kawaida katika mito na njia za maji nchini Nigeria. Mara nyingi, ajali hizo huhusishwa na boti kubeba watu kupita kiasi, matengenezo duni, na utekelezaji dhaifu wa kanuni za usalama. Idadi kubwa ya watu hupoteza maisha katika ajali hizo kila mwaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *