Mohammed Abdulsalam, Mkuu wa timu ya mazungumzo ya Yemen, amesisitiza kuwa tangazo la vikosi vya ulinzi vya Yemen kuhusu marufuku ya usafiri wa baharini dhidi ya Saudi Arabia ilikuwa hatua ambayo Sana’a ililazimika kuichukua kujibu hatua ya Riyadh kukataa kujibu kwa njia ya amani matakwa halali ya Yemen.

Kulingana na ripoti ya Jumatatu ya shirika la IRNA ikinukuu televisheni ya Al-Masirah, Mohammed Abdulsalam alieleza kupitia taraifa yake kwamba: “Saudi Arabia ilipewa fursa ya kutosha kutimiza wajibu wake kuhusiana na madhara ya uvamizi wake wa kikatili dhidi ya Yemen; na watu wa Yemen walivumilia mateso makubwa kwa matumaini ya kufikia suluhu kwa njia ya amani na kuepuka kuongezeka mapigano; hata hivyo utawala wa Saudi haukufanya lolote zaidi ya kuonyesha ukaidi, kuchelewesha muda na kukwepa ahadi zake.”

Mkuu wa timu ya mazungumzo ya Yemen amesema: Katika kipindi cha miaka minne iliyopita hususan tangu kusitishwa mapigano mwaka 2022 Saudi Arabia imejaribu kudhihirisha uchokozi wake wa miaka minane kama suala la ndani la Yemen ambalo halihusiki nalo, na hili limekuwa mojawapo ya vikwazo vikubwa katika kufikia suluhu ya pamoja.

Abdulsalam amesisitiza kuwa, ile dhana ya Saudi Arabia kwamba inaweza kuendeleza mzingiro dhidi ya Yemen kwa muda usiojulikana ni dhana potofu na kamari iliyofeli.  “Nchi yetu tukufu ilitoa kauli yake ya mwisho wakati wa maandamano makubwa ya Ijumaa iliyopita yaliyohudhuriwa na mamilioni ya watu na ambayo hayajawahi kushuhudiwa;l ikitangaza kuwa, muda uliotolewa kwa utawala wa Saudi umemalizika, na kwamba: Utawala wa Saudia unapasa kubeba dhima  ya madhara ya hatua yoyote ya kuongeza mvutano kutokana na kiburi chake, kwa sababu “mzingiro kwa mzingiro” ni jawabu la kawaida, la kisheria na la kimaadili dhidi ya ukaidi huo wa utawala wa Saudia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *