Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Jeshi la Marekani limesema limekamilisha usiku wa 11 mfululizo wa mashambulizi dhidi ya Iran, huku vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati vikizidi kudhoofisha juhudi za kidiplomasia za kusitisha mapigano.
Kamandi Kuu ya Marekani, inasema mashambulizi hayo yanalenga anga za ndege na maeneo ya kuhifadhi ndege zisizo na rubani. Mashambulizi hayo yanafanyika baada ya Rais Donald Trump kuashiria kuwa operesheni za kijeshi dhidi ya Iran zitaongezwa katika siku zijazo.
Wakati huo huo, Waziri wa mambo ya ndani wa Iran, Eskandar Momeni, anazuru Pakistan katika juhudi za kufufua mazungumzo ya kidiplomasia.
Hata hivyo, haijafahamika iwapo kutapatikana makubaliano mapya ya kumaliza vita ambavyo sasa vimejikita katika udhibiti wa Mlango wa Bahari ya Hormuz, njia muhimu inayotumika kusafirisha mafuta na gesi duniani.
Aidha, Trump amesema Marekani haina nia ya kufanya mazungumzo kwa sasa na kuashiria kuwa huenda vikosi vya Marekani vikapanua mashambulizi yake hadi maeneo yaliyo karibu na vituo muhimu vya nyuklia vya Iran.
Mvutano huo umeendelea kuathiri masoko ya nishati duniani, ambapo bei ya mafuta ghafi imepanda hadi zaidi ya Dola 92 kwa pipa huku gharama za mafuta zikiendelea kupanda katika baadhi ya nchi.