Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi, amemrudisha nyumbani kwake mjane Pendo Shija, aliyedaiwa kufukuzwa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mke mwenzake baada ya Mume wake kufariki MWANZONI MWA Mwaka huu.
Tukio hilo limetokea katika nyumba ya marehemu Steven Bernard Paulo, ambapo kwa miezi kadhaa kumekuwa na vuta ni kuvute baina ya wajane wawili ,Kila mmoja akidai kuwa ndiye mwenye haki ya kumiliki mali hiyo iliyoachwa na marehemu.
Baada ya kusikiliza pande zote , Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi amefika eneo la tukio Mtaa wa Igwambiti C Kata ya Lwanhuma na kwa kushirikiana na wananchi aliwaamuru kutoa mpangaji aliyekuwa ameletwa na upande wa pili, ili kumpisha mjane aliyefukuzwa wakati taratibu za miradhi zikiendelea.
Mkuu wa Wilaya amesisitiza kuwa mali ya marehemu isigawanywe kwa vurugu, bali ifuatwe utaratibu wa kisheria ili kuepuka uonevu baina ya wajane hao
Viongozi wa Mtaa wa Igwambiti C wanaeleza kumfahamu marehemu pamoja na mjane mmoja pendo Shija ambaye ameishi hapo kwa Zaidi ya Miaka mitano.
Wajane Hawa wawili wanaeleza kila mmoja kuwa na uhalali wa umiliki wa nyumba hiyo aliyoacha marehemu.
Hata hivyo kwa sasa Pendo Shija amerudi katika nyumba yake na anaendelea kuishi kwa amani huku taratibu za miradhi zikiendelea baina ya wanafamilia.
(Feed generated with FetchRSS)