Mtume wa Kanisa la Inuka Uangaze, Boniface Mwamposa amekutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Juma Mwenda.

Mkutano huo umefanyika leo katika ofisi za Makao Makuu ya TRA Jijini Dar es Salaam ambako pamoja na mambo mengine Mtume Mwamposa ameipongeza mamlaka hiyo kuboresha uhusiano mzuri uliopo baina ya TRA na walipakodi.

Mtume Mwamposa amesema kazi nzuri inayofanywa na TRA katika ukusanyaji wa kodi imetokana na kuimarika kwa uhusiano mzuri baina ya walipakodi na mamlaka hiyo huku na kuwatakq wafanyabiashara na wananchi wote kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi kwa hiari ili kuchangia maendeleo ya nchi.

Aidha, Mwamposa amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya maboresho makubwa katika mifumo ya kodi nchini na kuweka uongozi makini katika usimamizi wa kodi hali ambayo imeongeza imani zaidi ya Walipakodi kwa TRA.

Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Juma Mwenda amemshukuru Mtume Mwamposa kwa ulipaji kodi mzuri na kushiriki kuhamaisha ulipaji wa kodi kwa hiari huku akitoa wito kwa Walipakodi kuendelea kuiamini TRA na kulipa kodi kwa hiari.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *