Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) limetoa onyo kali kwa serikali ya kifalme ya Uingereza, likiitaja kuwa miongoni mwa nchi zilizokuwa na mchango mkubwa katika mashambulizi ya hivi karibuni yaliyofanywa na Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika taarifa yake, IRGC limesema Uingereza inapaswa kujiepusha na hatua zozote zitakazoongeza ushiriki wake katika hujuma na uchokozi dhidi ya Iran.

Jeshi hilo limesisitiza kuwa linaionya serikali ya kifalme ya Uingereza “isijiongezee mzigo wa lawama na kuzidi kuchafua faili lake,” likimaanisha kuwa kuendelea kuunga mkono au kushiriki katika hatua dhidi ya Iran kutakuwa na matokeo na kutazidisha wajibu wake kisiasa na kisheria.

Kitengo cha Uhusiano wa Umma cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimetoa taarifa kikitoa onyo kali kwa serikali ya Uingereza, kikisema kuwa London imekuwa miongoni mwa washirika wakuu wa mashambulizi ya hivi karibuni yaliyofanywa na Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika taarifa hiyo, jeshi la IRGC limesema Uingereza imechangia kwa kiwango kikubwa matatizo na migogoro inayowakumba wananchi wa eneo la Asia Magharibi, likisema pia kuwa historia yake inahusishwa na kugawa nchi za Kiislamu na kufanya mauaji makubwa katika mataifa mbalimbali ya eneo hili.

Jeshi hilo limeongeza kuwa, kutokana na ushiriki mkubwa wa Uingereza katika mashambulizi dhidi ya Iran, linaionya serikali ya kifalme ya nchi hiyo kutochukua hatua zozote zitakazoongeza wajibu wake katika mzozo huo, likisema: “Msiendelee kuchafua zaidi faili lenu na kulifanya kuwa zito zaidi dhidi ya Iran.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *