Hali ya usalama inaendelea kuzorota katika eneo la Mambasa katika mkoa wa Ituri, ambapo angalau raia 32 wameuawa na wengine kadhaa kutekwa nyara katika saa 72 zilizopita wakati wa mashambulizi mawili yaliyohusishwa na waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) katika vijiji vya Njiapanda-Bela na Lukaya.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na wanaharakati wa mashirika ya kiraia, vurugu hizi zimesababisha watu wengi kuhama makazi yao katika vijiji vilivyoathiriwa moja kwa moja na katika maeneo ya jirani, ambapo kusonga mbele kwa washambuliaji kunachochea hali ya hofu na kutokuwa na uhakika.

Shambulio la hivi karibuni liliripotiwa sik ya Ijumaa, Julai 24, huko Lukaya, ambapo watu saba waliuawa. Miili ya waathiriwa ilipatikana baada ya waasi kuondoka, huku wakazi kadhaa wakiripotiwa kuchukuliwa mateka. Masjirika ya kiraia nchini Kongo yanabainisha kuwa idadi hii ya vifo ni ya muda, huku utafutaji unaendelea kwa waathiriwa wengine wowote.

Siku mbili mapema, washambuliaji hao walilenga kijiji cha Njiapanda-Bela. Baada ya idadi ya vifo vya muda ya watu 16 kuripotiwa na mashirika ya kiraia, miili zaidi iligunduliwa, na kufanya idadi ya waliouawa kufikia 25. Wakazi kadhaa pia walitekwa nyara na kulazimishwa kubeba nyara zilizoibwa na waasi hadi msituni.

Kulingana na taarifa zilizotolewa na mashirika ya kiraia, wapiganaji wa ADF sasa wanaelekea Makumo, na kuwafanya wakazi wengi kukimbia makwao kwa kuhofia mashambulizi zaidi. Hali ya hofu pia inaripotiwa katika eneo la Malulu, lililoko katika eneo jirani la Irumu, hasa katika eneo la Tchabi, ambapo tishio la ADF linabaki kuwa jambo la kutia wasiwasi mkubwa, kwani idadi ya watu wanaishi kwa hofu ya shambulio linalowezekana la kundi hili lenye silaha.

Wito wa kuingilia kati kwa haraka kijeshi

Kutokana na kuibuka tena kwa vurugu, wanaharakati wa mashirika ya kiraia huko Mambasa wanaitaka serikali kuimarisha uwepo wa kijeshi katika eneo hilo na kuwapa wanajeshi uwezo na vifaa vinavyohitajia zohitajika ili kuwaangamiza kabisa ADF.

Wanasema kwamba tangu mwezi Machi 2026, kundi hili lenye silaha limeripotiwa kuwaua zaidi ya watu mia moja katika vijiji ishirini katika eneo la Mambasa.

“Tunawasihi viongozi kuchukua suala la ADF kwa uzito. Waasi hawa wanaua na kuhujumu juhudi za serikali,” alitangaza Marie-Noëlle Anotane, mwanachama wa mashirika ya Kiraia ya Kongo.

Mashirika ya kiraia pia yanawasihi raia kushirikiana kwa karibu na idara za usalama ili kuwezesha mapambano dhidi ya makundi yenye silaha. Hasa, yanawasihi wale wanaoshukiwa kuunga mkono au kushirikiana na ADF kukomesha aina zote za ushiriki na harakati hii, ambayo inawajibika kwa ukosefu wa usalama unaoendelea katika maeneo kadhaa ya Ituri.

Kufikia Jumamosi jioni, wala mamlaka zaeneo hilo wala Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hazikuwa zimejibu rasmi mashambulizi haya mapya. Hata hivyo, watu walioathiriwa wanatumai kuingilia kati haraka ili kuzuia mauaji zaidi na kuwezesha kurejea kwa usalama katika sehemu hii ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *