MCHEZAJI wa Mlandege, Mudathir Juma Salum ‘Park’ amesema msimu wa 2025-2026 ulikuwa sehemu ya kujifunza na kuzoea mazingira lakini msimu ujao wa 2026-2026 atapambana kuhakikisha anapata namba kikosi cha kwanza.

Amesema licha ya msimu uliopita kutopata nafasi ya kucheza, wala hajakata tamaa zaidi ya kuongeze bidii kufanya mazoezi kwa lengo la kujiweka fiti kwa ajili ya msimu ujao.

“Nashukuru msimu wa 2025-2026 ulikuwa mzuri kuanzia siku ya kwanza nafika hadi sasa napewa ushirikiano mkubwa ndani na nje ya uwanja, najivunia kuwepo Mlandege,” amesema.

Alibainisha timu hiyo haijamuathiri zaidi ya kujifunza mengi kwani nyakati katika maisha hazifanani na subira na uvumilivu ndiyo inayohitajika kila hatua.

Hivyo, amesema amejipanga kuhakikisha anapambana kupata namba katika kikosi cha kwanza ndiyo maana anafanya mazoezi binafsi kila siku.

Amesema anaamini msimu ujao utakuwa bora zaidi kwa sababu ameshajua anachotakiwa kukiongeza, hivyo anapambana kumshawishi kocha ampe nafasi kutokana na kile atakachokionesha mazoezini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *