Wapalestina wengine tisa wameuawa shahidi katika mashambulizi ya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza katika saa 24 zilizopita.

Wizara ya Afya ya Gaza imeripoti kuwa, tangu Oktoba 7, 2023 hadi sasa Israel imeuwa shahidi Wapalestina 73,326 katika eneo hilo.

Taarifa ya wizara hiyo imeeleza kuwa hospitali za Gaza zimepokea miili ya wahanga tisa, wakiwemo Wapalestina saba waliouawa katika saa 24 zilizopita, na wawili walioaga dunia kutokana na majeraha waliyopata katika mashambulizi ya karibuni ya Israel.

“Watu 36 waliojeruhiwa wamelazwa hospitalini na hivyo idadi ya majeruhi kufikia 173,997,” imeongeza taraifa ya Wizara ya Afya ya Gaza.

Miili ya watu wengi ingali imenaswa chini ya vifusi na barabarani, huku magari ya wagonjwa na kikosi cha ulinzi wa raia vikishindwa kuwafikia kutokana na mashambulizi yanayoendelea ya Israel.

Takwimu za Wizara ya Afya ya Gaza zinaonyesha kuwa licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyoanza kutekelezwa tarehe 10 Oktoba 2025, jeshi la Israel limeendelea kuwashambulia Wapalestina kila siku; ambapo hadi sasa Wapalestina wasiopungua 1,200 wameuawa shahidi na 3,888 kujeruhiwa huko Gaza.

Vita vya Israel vilivyonza Oktoba mwaka 2023  hadi sasa vimesababisha uharibifu mkubwa katika Ukanda wa Gaza na hali mbaya kibinadamu kwa wakazi wa eneo hilo milioni 2.4.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *