Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atampokea mwenzake wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, katika Ikulu ya Élysée leo Jumatano, Agosti 27. Ziara hii ya kiserikali inatarajiwa kufunguwa ukurasa mpya ya uhusiano kati ya Ufaransa na Senegal.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Dakar, Juliette Dubois

Mkutano huo utaanza leo Jumatano, Agosti 27, saa 2:30 asubuhi huku Emmanuel Macron akimpokea rais wa Senegal katika Ikulu ya Élysée. Mkutano huu unafanyika katika muktadha wa kipekee: kusawazisha upya uhusiano kati ya Ufaransa na Afrika, ulioshuhudiwa nchini Senegal kwa kufungwa kwa kambi za mwisho za kijeshi za Ufaransa miezi miwili iliyopita.

Kulingana na wasaidizi wa Bassirou Diomaye Faye, “masuala yote yatajadiliwa.” Katika ajenda: faili ya ukumbusho ya Thiaroye. Huko Dakar, kwa muda mrefu kumekuwa na wito kwa Ufaransa kukabidhi nyaraka zake zote za kijeshi na kimahakama katika mauaji ya mwezi Desemba 1944. Senegal sasa inadai kutengwa kabisa kwa hati zilizoainishwa zilizosalia na kutambuliwa kwa idadi halisi ya wahasiriwa.

Ufaransa bado ni mwekezaji mkuu nchini Senegal…

Masuala makubwa ya kiuchumi pia yanatarajiwa kuwa mezani, hasa mzozo wa deni la treni ya mxwendo kasi ya mkoa wa Dakar–Diamniadio, ambayo kampuni ya Eiffage inadai takriban euro Milioni 150. Maendeleo endelevu, elimu, na masuala ya afya pia yatajadiliwa, kwa lengo lililoelezwa la kujenga ushirikiano unaoitwa “kunufaika kwa pande zote”, kwa kuzingatia zaidi vipaumbele vya Senegal.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya rais wa Ufaransa, wakuu hao wa nchi pia wanatarajiwa kushughulikia migogoro ya kikanda na masuala makubwa ya kimataifa. Hatimaye, ikumbukwe kwamba Bassirou Diomaye Faye atashiriki, kama mgeni maalum, katika mkutano wa wafanyabiashara wa Ufaransa ulioandaliwa na Medef, shirika kuu la waajiri wa Ufaransa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *