#HABARI: Jeshi la Polisi nchini, limetoa tamko kuelekea uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu zinazotarajiwa kuzinduliwa kuanzia …#HABARI: Jeshi la Polisi nchini, limetoa tamko kuelekea uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu zinazotarajiwa kuzinduliwa kuanzia …

#HABARI: Jeshi la Polisi nchini, limetoa tamko kuelekea uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu zinazotarajiwa kuzinduliwa kuanzia kesho Agosti 28, 2025.

Jeshi hilo limewaambia wananchi na wadau wote kuwa, lipo tayari na limejiandaa vizuri ipasavyo kuhakikisha linaendelea kuimarisha usalama wakati wote wa kampeni na baada ya kampeni.

Aidha, Jeshi la Polisi limetoa wito kwa Wagombea na wafuasi wao na Wananchi wote kwa ujumla, kukumbuka kuwa, jukumu la kudumisha Amani, Utulivu na Usalama ni letu sote kama Watanzania na kamwe asiwepo mmoja wetu akawa chanzo cha kukiuka Sheria, Kanuni na Taratibu wakati wote wa kampeni na baada ya kampeni ili kuepuka vurugu au uhalifu wa aina yoyote ile kutokea.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *