
Mauzo ya bidhaa za Iran kwa nchi za Asia Magharibi yameongezeka katika mizei ya hivi karibuni.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Asia Magharibi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Biashara ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Mauzo ya Iran nje ya nchi yameongezeka katika nusu ya kwanza ya mwaka huu kwa nchi za eneo zikiwemo Uturuki, Qatar, Oman na Bahrain.
Abdol Amir Rabihavi, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Magharibi mwa Asia ya Shirika la Maendeleo ya Biashara la Iran amesema: “Kwa kuzingatia takwimu, mauzo ya nje katika nchi za Asia Magharibi zikiwemo Uturuki, Qatar, Oman na Bahrain yameshuhudia ongezeko la asilimia 8 hadi 9 katika miezi sita ya mwanzo ya mwaka huu, jambo ambalo linaashiria mwelekeo mzuri wa biashara ya nje ya Iran katika eneo hili.”
Rabihavi amesema kuwa jumla ya biashara ya nchi za Asia Magharibi ni zaidi ya dola bilioni 237 na kuongeza: “Hivi sasa, hisa ya Iran katika takwimu hizi ni chini ya asilimia moja, lakini tunayo ramani ya wazi ya kuongeza hisa hii. Lengo letu la biashara na Uturuki ni dola bilioni 30, Iraq $20 bilioni, na Oman $5 bilioni.” Ukuaji wa biashara ya Iran na mataifa mengine unashuhudiwa katika hali ambayo, katika miaka ya hivi karibuni taifa hili limekuwa likiandamwa na vikwazo vya kidhalimu vya Marekani na washirika wake.