#HABARI: Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Salim Alaudin Hasham, amepokelewa na wananchi pamoja na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo hilo kupitia tiketi ya CCM.
Akichukua fomu hiyo katika ofisi za tume huru ya uchaguzi, Salim ametaja vipaumbele atakavyohakikisha Serikali inakamilisha ni pamoja na kujenga hospitali ya wilaya itakayokidhi ongezeko la wananchi, ujenzi wa skimu za umwagiliaji katika maeneo ya Lupiro, Lukande, Iyoga na Minepa pamoja na ujenzi wa barabara kutoka Ifakara hadi Mahenge kwa kiwango cha lami.
Salim amechukua fomu hiyo Agosti 26, na kuahidi kuisimamia na kuitekeleza ilani ya CCM endapo atapata nafasi hiyo.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania
