
Al-Shabaab walikuwa wakilenga gereza la “Godka Jilicow” wanakozuiliwa baadhi ya wanamgambo wa kundi hilo. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Somalia imetangaza kuwa shambulio hilo lililofanyika karibu na Ikulu ya rais, lilidumu kwa saa kadhaa, lakini vikosi vya usalama vilifanikiwa kuzima shambulio hilo la kigaidi kwa kuwapiga risasi watu saba waliokuwa wamejihami kwa bunduki.
Hali ya usalama inazidi kuwa mbaya katika nchi hiyo maskini na isiyo na utulivu katika Pembe ya Afrika kufuatia kuibuka tena kwa kundi hilo la al-Shabaab lenye mafungamani na kundi la Kigaidi la al-Qaeda.