
Kiongozi wa siasa kali za mrengo wa kulia nchini Ufaransa Marine Le Pen amesema leo Jumatatu kwamba kuvunjwa kwa Bunge la taifa “hakuwezi kuepukika kabisa,” kufuatia kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Sébastien Lecornu, chini ya siku moja baada ya kuunda serikali yake.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Itakuwa “busara” kwa Rais Emmanuel Macron kujiuzulu, ameongeza, chaguo ambalo hapo awali lilikataliwa na mkuu wa nchi.
Hayo yanajiri wakati Sébastien Lecornu amejiuzulu kwenye wadhifa wake wa waziri mkuu. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekubali hatua ya Waziri wake Mkuu Sebastien Lecornu kutangaza kujiuzulu saa chache baada ya kulitaja baraza lake la Mawaziri kulingana na taarifa kutoka kwa Ofisi ya Rais.
Kulingana na wachambuzi wa kisiasa, hatua hii inalitumbukiza zaidi taifa hilo la Ulaya kwenye mkwamo wa kisiasa.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alimteua Lecornu, Waziri wa zamani wa ulinzi kwenye wadhifa huo mwezi uliopita.
Lecornu alikuwa anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuja na bajeti ya mwaka ujao, itakayokubaliwa na bunge.