Mazungumzo kati ya serikali ya Jamhuri ya kidemoktrasia ya Congo na waasi wa AFC/M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, yanatarajiwa kufanyika wiki hii chini ya upatanishi wa Qatar, kwenye mji wa Doha.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Vyanzo mbali mbali vinasema wajumbe kutoka pande hizo mbili wanatazamiwa kujaribu kutatua baadhi ya vikwazo, hasa zaidi suala la kubadilishana wafungwa wa kisiasa, ambalo linazingatiwa na uasi kuwa mojawapo ya masharti muhimu kwa maendeleo yoyote katika mazungumzo hayo, huku serikali ya Kinshasa ikiendelea kusisitizia mpango wa kuwaondoa wanajeshi wa Rwanda RDF wanaowasaidia waasi hao.
Hata hivyo, mvutano umesalia kuwa mkubwa huko Kivu Kaskazini na Kusini, ambako pande zote mbili zinaendelea kuimarisha misimamo yao.

Wajumbe kutoka serikali ya Kinshasa na AFC/M23 wanatarajiwa wiki hii mjini Doha, Qatar, kwa awamu mpya ya majadiliano chini ya upatanishi wa Qatar lakini matumaini ya kufikia mwafaka kwa awamu ni finyu sana.
Tayari utaratibu wa baadhi ya vipengele vilivyokubaliwa na pande zote mbili katika mchakato huu wa Doha, umetiwa saini ili kukabidhi Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) jukumu la mpatanishi huru anayehusika na kutambua,kuthibitisha na kuwezesha kuachiliwa kwa wafungwa hao.