Mpango huo unajumuisha pia kuachiliwa kwa mateka wa Israel na wafungwa wa Kipalestina miongoni mwa mambo mengine.  Mazungumzo hayo  yaliyoanza Jumapili chini ya mpango wa amani uliopendekezwa na rais wa Marekani Donald Trump, yanaonyesha dalili za kufanikiwa huku yakiungwa mkono na viongozi mataifa mbalimbali duniani.

Akiondoka nchini Qatar, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Johann Wadephul ataelekea Misri na Israel ambapo anatarajiwa kuzungumza na viongozi wa nchi hizo kuhusu mpango huo wa amani ambao ameusifia.

Kowait | Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Johann Wadephul
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Johann Wadephul akiwa na viongozi wa nchi za Ghuba huko KoweitPicha: Soeren Stache/dpa/picture alliance

” Ukweli ni kwamba hakuna mpango bora zaidi kuliko wa Rais Trump. Ni lazima utekelezwe kikamilifu, hata kama baadhi ya vipengee vinahitaji kufafanuliwa. Lakini kuna uwezekano mateka wakaachiliwa hivi karibuni, kukafikia usitishaji wa mapigano huku watu wanaoteseka  Gaza  wakipata msaada wa kutosha wa kibinadamu. Itakuwa hatua ya kwanza ya matumaini inayoweza kufikiwa katika siku chache zijazo na ni matumaini yangu kuwa itafanikiwa.”

Baadaye Wadephul ataelekea Kuwait kushiriki mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya na Baraza la Ushirikiano la nchi za Ghuba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *