
Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu, Oktoba 6, Baraza la Kitaifa la Maaskofu wa Kanisa Katolika nchini DRC (CENCO) limesema linasikitishwa na hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya rais wa zamani Joseph Kabila. Baraza hilo limeonyesha upinzani wake kwa matumizi ya hukumu ya kifo nchini DRC.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Katiba ya nchi yetu inazingatia utakatifu wa maisha ya binadamu na inahesabu kuwa ni miongoni mwa haki za kimsingi ambazo haziwezi kukiukwa kwa hali yoyote ile. Hakika, utekelezaji wa hukumu ya kifo ni ukiukwaji wa haki ya kuishi inayotetewa na Kanisa kwa kuzingatia sheria ya Mungu: “Usiue,” Kutoka 18,” amesema Askofu Donatien Nshole, Katibu Mkuu wa CENCO katika video inaosambaa.
Kwa mujibu wa maaskofu wa Kikatoliki, hukumu ya kifo na mantiki yake ya kulipiza kisasi haiungwi mkono na Injili ya Kristo. CENCO inasema “imeshtushwa na hukumu ya Mahakama Kuu ya Kijeshi ya Kinshasa kufuatia kesi ya jinai iliyoanzishwa dhidi ya rais wa wa zamani Joseph Kabila, na kumhukumu adhabu ya kifo.”
Mnamo Machi 23, 2024, chanzo hicho kilikumbusha, kufuatia waraka wa Waziri wa Sheria kuhusu kufutwa kwa sheria inayopiga marufuku adhabu ya kifo. CENCO ilitoa wito wa kujitolea kutetea maisha na kukomesha hukumu ya kifo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
“Kwa hiyo, kusitishwa kwa utaratibu huo kwa asili kunatakiwa kupelekea kukomeshwa kwa adhabu ya kifo na si kurejesha adhabu hiyo kwa hatua isiyo ya kibinadamu, na jambo lingine inaonesha kushindwa kwa upande wa jamii , inadhalilisha utu wa binadamu aliyeumbwa kwa sura ya Mungu,” alisisitiza Askofu Nshole.