
Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani imethibitisha leo kuwa watu hao wamepelekwa nchini Ugiriki, ambako walipokelewa na wafanyakazi wa ubalozi wa Ujerumani.
Wiki iliyopita, jeshi la majini la Israel lilizivamia na kuziteka meli 42 zilizokuwa zikisafirisha misaada ya kibinadamu kupitia Bahari ya Mediterania kuelekea Ukanda wa Gaza.
Zaidi ya watu 400 kutoka mataifa mbalimbali walitiwa nguvuni katika tukio hilo ambalo limezua mjadala mkubwa kimataifa.
Miongoni mwa waliokamatwa ni mwanaharakati maarufu wa mazingira kutoka Sweden, Greta Thunberg, na aliyekuwa meya wa jiji la Barcelona, Ada Colau.