Wafanyabiashara wadogo wa mipakani, hususan wanawake na vijana wanaouza mbogamboga, matunda na mazao ya nafaka, wamekutana na wadau wa sekta za umma na binafsi kujadili changamoto zinazokwamisha biashara zao.

Mkutano huo una lengo la kuondoa vikwazo visivyo vya kiforodha na kuimarisha biashara katika maeneo ya mipakani, baada ya kubainika kuwa licha ya juhudi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kupunguza ushuru wa forodha, bado kuna changamoto zisizo za kiforodha kama ucheleweshaji wa mizigo, taratibu zisizoratibiwa na upungufu wa uelewa kuhusu nyaraka za viwango vya biashara.

Majadiliano haya yanayofanyika mpaka wa Taveta-Holili mkoani Kilimanjaro yameandaliwa na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Ukuaji Endelevu wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRA) na wadau wengine, yakiwa na lengo la kukuza biashara ya bidhaa za kilimo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

✍ Ramadhani Mvungi
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *