
Mashariki ya DRC, zaidi ya asilimia 80 ya vituo vya afya vimemaliza dawa zake muhimu katika eneo hilo ambalo linaendelea kukabiliwa na mapigano kulingana na ripoti ya shirika la kimataifa la msalaba mwekundu ICRC.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa kipindi cha miaka 30, eneo hilo lenye utajiri wa mafuta limekuwa likikabiliwa na machafuko, mapigano yakiongezeka mwaka huu ambapo kundi la waasi wa M23 linaloungwa mkono na Rwanda limechukua udhibiti wa Miji ya Goma na Bukavu.
Mapigano kati ya waasi wa M23 na jeshi la serikali ya Congo yamesababisha vifo vya maelfu ya raia wakati mamilioni ya wengine wakipoteza makazi yao tangu mwezi Januari.
Tangu Rwanda na DRC zitie saini makubaliano ya amani yalioongozwa na Marekani mwezi Juni, utekelezwaji wake umekuwa ukijikokota.
Mwezi Septemba, ICRC iligundua kuwa vituo vya afya 240 katika maeneo ya Kivu Kusini na Kaskazini ambapo mapigano yanaripotiwa vilikuwa vikifanya kazi tangu mwezi Machi licha ya changamoto zilizopo.
Zaidi ya asilimia 85 ya vituo hivi vilishuhudia kukabiliwa na upungufu wa usambazaji wa dawa wakati asilimia 40 kati ya vituo hivyo vikikosa idadi ya wahudumu wanaohitajika, kulingana na ripoti ya ICRC.
ICRC imesema hatua hii inatokana na machafuko yanayoendelea mashariki ya Congo ambapo sehemu kubwa ya mashirika ya misaada yamesisitisha shuguhuli zao kwa kuhofia usalama wa wafanyikazi wake.
Aidha ICRC inasema idadi kubwa ya watu waliojeruhiwa wanafika katika vituo hivyo vya afya kupata matibabu ila wanakosa dawa zinazohitajika kwa ajili ya kupewa huduma za kiafya.
Zaidi ya asilimia 70 ya vituo hivyo viliwasajili watu waliokuwa wamejeruhiwa kutokana na mapigano yanyoendelea mashariki ya DRC tangu kuanza kwa mwaka huu, ilisema ripoti ya ICRC.