Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Juma Mkomi ametoa wito kwa watumishi wa umma kote nchini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu.

Akizungumza jijini Dodoma wakati wa kikao cha tatu cha Baraza la Nane la Wafanyakazi, Mkomi amesema ni jukumu la kila Mtanzania mwenye sifa ya kupiga kura kuhakikisha anashiriki kikamilifu katika mchakato huo wa kidemokrasia.

Ameongeza kuwa hata viongozi wa kisiasa wamekuwa wakihamasisha familia zao kushiriki uchaguzi, hivyo ni vyema kwa watumishi wa umma kuwa mfano wa kuigwa kwa kushiriki kwa amani na utulivu.

Kauli hiyo inakuja wakati taifa likijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, mwaka huu.

✍ Mwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *