Homa ya Uchaguzi Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imezidi kupamba moto baada ya Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo, Oktoba 10, 2025 kutangaza orodha ya awali ya wagombea waliorejesha fomu.

Kutangazwa kwa orodha hiyo kunafungua mlango kwa zoezi la usaili lililopangwa kufanyika Oktoba 15, 2025 Dar es Salaam.

Lugano Josseah, Mwenyekiti Namungo FC

Taarifa iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Benjamin Kalume imeeleza kuwa wagombea hao ni wa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wawakilishi wa klabu

Nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi, majina matatu yametajwa ambayo ni Nassor Idrissa Muhamed, Said Soud Said, na Hoseah Hopaje Lugano.

Nassor Idrissa, Rais wa Azam FC

Idrissa ni Rais wa Azam FC huku Lugano akiwa ni mwenyekiti wa Namungo FC na Soud anawania nafasi hiyo akiwa ni mwenyekiti Mtibwa Sugar.

Wagombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Kheri Nassor Missinga na Hassan Ramadhan Muhsin ambao watachuana kuwania nafasi hiyo muhimu ya kusaidiana na mwenyekiti katika uendeshaji wa shughuli za ligi.

Said Soud, Mwenyekiti Mtibwa Sugar
 

Kwa wawakilishi wa klabu za Ligi Kuu, majina mawili yametajwa ambayo ni Japhet Mboto Makau na Gilbert Morice Nkoronko.

Katika kundi la Ligi ya Championship, wawakilishi waliorejesha fomu ni Hillary John Ndumbaro na Ahmed Waziri Gao.

Kutoka First League, jina pekee lililotajwa ni la Azimkhan Akber.

Uchaguzi Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania umepangwa kufanyika, Novemba 29, 2025 hapa Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *