Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) limeitaka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kuhakikisha inaendelea kuboresha mikakati ya mtangamano wa kikanda, hasa katika maeneo ya mipakani, ili kuondoa changamoto za mwingiliano wa biashara.

Rai hiyo imetolewa na wabunge wa EALA walipotembelea taasisi hiyo jijini Arusha, wakiongozwa na Dkt. Abdullah Makame kutoka Tanzania, katika ziara ya kutathmini mchango wa taasisi za elimu ya juu katika maendeleo ya kikanda.

Profesa Antony Mshandete, Naibu Makamu Mkuu wa taasisi hiyo, amesema wabunge wanataka chuo hicho kuchangia ubunifu unaoongeza thamani ya mazao na kuimarisha mtangamano wa kibiashara.

✍ Ramadhani Mvungi
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *