Mgombea Ubunge Jimbo la Kibamba kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi ( CCM ), Angellah Kairuki amesema akichaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo, atahakikisha huduma ya maji pamoja na afya zinaboreshwa, hususani katika eneo la afya ya mama na mtoto.

Alifafanua kuwa, maboresho hayo yataendana sambamba na ujenzi wa zahanati na vituo vya afya kwenye mitaa ambayo haina huduma hizo.

‎Kairuki amesema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyia Kata ya Kwembe katika mwendelezo wa Kampeni zake kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanya Oktoba 29 mwaka huu.

Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *