Jeshi lachukua nchi Madagascar
Jeshi la Madagascar limechukua mamlaka ya nchi hiyo, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumanne na kanali wa jeshi, baada ya Rais Andry Rajoelina kukimbilia ughaibuni kufuatia mvutano kati yake na waandamanaji wa Gen Z na vikosi vya usalama.