Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga amefariki dunia leo Oktoba 15, 2025 akipatiwa matibabu huko Kochi nchini India.

Kwa mujibu wa msemaji wa hospitali ya Ayurvedic, Hayati Odinga alipata mshtuko wa moyo wakati akifanya matembezi ya asubuhi ndani ya majengo ya kituo cha Ayurvedic na kukimbizwa katika Hospitali ya Devamatha iliyopo Koothattukulam, ambako alitangazwa kuwa amefariki saa 9.52 asubuhi.

Odinga aliyefariki akiwa na umri wa miaka 80, atakumbukwa kama mwanasiasa mashuhuri, aliyehubiri mageuzi na umoja wa kitaifa, ambaye amehudumu kama waziri mkuu wa Kenya kati ya 2008 hadi 2013.

Historia pia inamuandika Odinga kama mgombea urais mara nyingi zaidi akifanya hivyo mara tano kuanzia 1997, 2007, 2013, 2017 na 2022, licha ya mara zote kutofanikiwa kushinda; lakini ameweka alama ya kuwa mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa na wafuasi wengi zaidi nchini humo.

✍ @abuuyusuftz

#RIPRailaOdinga #RailaOdinga #Odinga #Baba

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *