#HABARI: Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kenya (KCAA) imewatangazia wananchi kuwa shughuli za ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) zimesitishwa kwa muda kufuatia tukio la kiusalama linaloendelea baada ya kuwasili kwa mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Rt. Hon. Raila Odinga.
Taarifa rasmi ya KCAA imeeleza kuwa idadi kubwa ya waombolezaji wamevamia maeneo ya uwanja yaliyozuiliwa, hali iliyolazimu kufungwa kwa tahadhari ili kutoa nafasi kwa vikosi vya usalama kurejesha utulivu na kuhakikisha usalama kwa wote walioko uwanjani.
Wananchi na wasafiri wametakiwa kutulia na kuepuka eneo la JKIA hadi watakapopata taarifa zaidi. KCAA imesema shughuli za kawaida zinatarajiwa kurejea baada ya saa mbili mara baada ya hali kutangazwa kuwa salama.
Taarifa ya NOTAM (Notice to Airmen) imetolewa rasmi kuhusu kufungwa kwa muda kwa uwanja huo. KCAA imeomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na kushukuru kwa ushirikiano na uvumilivu wa wananchi.
•Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania