#HABARI: Utafiti unaoendelea kufanyika katika Kitalu cha Lindi–Mtwara, mkoani Mtwara umeonesha dalili za uwepo wa Gesi Asilia, hususani katika Vijiji vya Mnyundo na Mpapura, ambapo visima vya maji vilibainika kuvujisha gesi asilia.
Utafiti huo unajumuisha jumla ya vijiji 48 katika eneo la takribani kilomita za mraba 736 ambapo vijiji 40 vinatoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara (Mtwara DC) na Vijiji 8 ni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mtama (Mtama DC).
Katika ziara yake ya kukagua miradi ya gesi na mafuta mkoani Mtwara, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio, amesema kuwa utafiti wa awali unaonesha uwezekano mkubwa wa kupatikana kwa gesi asilia katika eneo hilo.
“Kwa kutumia data za mitetemo zilizokusanywa awali, tumebaini kwamba kuna hadi asilimia 32 ya uwezekano wa gesi kuwepo katika kitalu hiki” Amesema Dkt. Mataragio.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.