Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewahakikishia wakazi wa jiji hilo kuwa mazingira ya kupiga kura yatakuwa salama na amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la kupiga kura litakalofanyika tarehe 29 mwezi huu.

Akizungumza katika mkutano uliozikutanisha Mama lishe, Baba lishe, vijana, wanawake, bodaboda, machinga na wadau mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam, Chalamila alisema jiji hilo lina jumla ya wapigakura zaidi ya milioni nne na wote wako huru kushiriki bila hofu.

Chalamila amesisitiza kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani, huku akihimiza makundi yote ya kijamii kushiriki kikamilifu ili kuchagua viongozi wanaowataka kwa uhuru na utulivu.

Mhariri @claudJM
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *