
Kulingana na uchambuzi wa shirika la habari la AFP na pia data kutoka shirika la ACLED, hali hiyo imesababisha vifo vya watu 77,000.
Mashirika hayo yameongeza kuwa makundi yenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda yanafanya mashambulizi kote eneo hilo kuanzia Mali, Burkina Faso, Niger, Nigeria hadi mipaka ya Senegal.
Charlie Werb, mchambuzi katika shirika la ACLED ametahadharisha kuwa mzozo wa usalama katika kanda ya Sahel ni tete na hakuna suluhisho la haraka.
Hivi karibuni, Umoja wa Mataifa ulikadiria kuwa mtandao wa Al-Qaeda pamoja na Kundi linalojiita Dola la Kiislamu (IS) wana kati ya wanamgambo 7,000 na 9,000 katika kanda hiyo huku Kundi jingine kwa jina ISWAP likiwa na kati ya wanamgambo 8,000 na 12, 000.