#HABARI:Mgombea Mwenza nafasi ya Makamu wa Rais wa Chama cha Umma (CHAUMMA) Mhe Devotha Minja, ametangaza CHAUMMA Zanzibar Inamuunga mkono Mgombea wa nafasi ya urais Zanzibar kupitia ACT Wazalendo Mhe. Masoud Othaman.

Minja ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Micheweni Pemba, ambapo amesema CHAUMMA haijaweka Mgombea wa urais kwa upande wa Zanzibar kwa kutambua mchango wa Hayati Maalim Seif, katika kupambania haki kwa wananchi wa Pemba.

Amesema CHAUMMA wapo tayari kushirikiana na ACT Wazalendo kwa upande wa Zanzibar, Iła kwa upande wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamuunge mkono Mgombea wa CHAUMMA Mwalimu Salum Juma, kuwa Rais kwa kumpa kura nyingi za kutosha aongoze nchi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *