#HABARI: Polisi wa Korea Kusini wamesema wanatafuta kibali cha kumkamata mwanamke aliyesababisha moto katika makazi yake wakati akijaribu kumuua mende.
Jirani mmoja wa mwanamke huyo alipoteza maisha baada ya kuanguka kutoka ghorofani katika jaribio lililoshindikana la kujaribu kujiokoa na moto huo kupitia dirisha.
Mwanamke huyo, ambaye yuko katika umri wa miaka ya ishirini, aliwaambia polisi kuwa alijaribu kuchoma mende kwa kutumia kiberiti na dawa inayowaka moto, na kuongeza kuwa amewahi kutumia mbinu hiyo hapo awali.
Hata hivyo, siku ya Jumatatu, baadhi ya vitu ndani ya nyumba yake vilishika moto.
Polisi katika Jiji la Kaskazini la Osan wamesema mwanamke huyo anaweza kufunguliwa mashtaka ya kusababisha moto kwa bahati mbaya na kusababisha kifo kwa uzembe.
Kuchoma mende kwa kutumia vifaa vya kulipua moto iwe ni tochi au vifaa vya kutengeneza moto nyumbani kumekuwa mbinu mpya ya kuondoa wadudu wa nyumbani, ikienezwa kupitia video katika mitandao ya kijamii.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania