#HABARI: Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Kusini, Mtwara imewahukumu kunyongwa hadi kufa mapacha wawili Daniel Stephen Seif (Kurwa) (24) mkulima, mkazi wa Kijiji cha Mraushi “A” Wilaya ya Masasi na Daniford Stephen Seif (24) (Doto) mkulima Mkazi wa Kijiji cha Mraushi “A” Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, baada ya kupatikana na hatia ya mauaji kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16, kifungu cha 196 na 197 marejeo ya Mwaka 2022.

Daniel na Daniford wote kwa pamoja walitenda kosa hilo Disemba 15, 2024 katika Kijiji cha Mraushi “A” kwa kumpiga mama yao mzazi Upendo Methew (42), katika paji la uso, kwa kutumia jembe na mchi hivyo kumsababishia majeraha yaliyopelekea kifo chake.

Watiwahatiani wote wawili walikiri kutekeleza mauaji hayo ya kikatili baada ya kumtuhumu mama yao kuwa anawaroga.

Hukumu hiyo imetolewa Septemba 11, 2025 na Mahakamu Kuu Kanda ya Kusini Mtwara mbele ya Mhe.Jaji wa Mahakama Kuu Martha Mpaze na Mawakili wasomi Justus Revocatus Zegge na Dais Makakala.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *