#HABARI: Wasimamizi wa uchaguzi katika Jimbo la Kigoma Kaskazini wamewataka wapiga kura katika jimbo hilo kuhakikisha wanapiga kura kwa amani na kuwa na imani na vyombo vilivyowekwa kusimamia uchaguzi huo kwa kuwa watatenda haki katika kuhakikisha amani inalindwa kwa masilahi ya nchi na watu wake.

Bi. Happiness Ngagabale ambaye ni Afisa Uchaguzi Jimbo la Kigoma Kaskazini pamoja na Bw. Linus Kainda ambaye ni msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo wamesema hayo wakati wa mafunzo kwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *