#HABARI: Mgombea Ubunge Jimbo la Bukombe kupitia Chama Cha Mapunduzi (CCM) Dkt. Doto Biteko, amewashukuru wana Bukombe kwa heshima waliyompa kipindi chote cha kampeni katika Wilaya ya Bukombe.

Dkt. Biteko ametoa shukrani hizo wakati wa kuhitimisha kampeni katika Uwanja wa Igulwa, wilayani Bukombe, mkoani Geita.

“Nataka niwaambie wana Bukombe huwa mnanipa deni kubwa sana moyoni mwangu hamjui tu, huwa hamjui huwa najiona mmenipa stahili nisiyostahili kwa sababu kama binadamu nina mapungufu yangu mengi lakini mnanipa heshima, nitafanya kila linalowezekana vijana wa hamasa wasiishie kwenye kampeni ni vijana wetu lazima tuwakomboe, nataka niwaambie kila wakati tukiwaita mnakuja mnanipa deni na heshima kubwa sana”

Dkt. Biteko amewashukuru pia vijana wa hamasa na kuahidi kuwapa ushirikiano wa hali na mali.

Dkt. Biteko amewakumbusha wana Bukombe kuwa leo ilikuwa siku ya kuhitimisha kampeni katika jimbo la Bukombe na tarehe 29 wajitokeze kwa wingi vituoni kupiga kura kwa wagombea wote wa CCM, Ili Chama hicho kiendelee kuwa madarakani.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *