#HABARI: Mhandisi Godfrey Kasekenya, mgombea Ubunge wa jimbo la Ileje mkoani Songwe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amehitimisha kampeni zake katika kata ya Itale huku akiahidi kufanya maboresho makubwa ya huduma za kijamii endapo ataaminiwa tena na wananchi kumwakilisha bungeni.
Akihutubia wakazi wa eneo hilo, Kasekenya ameelezea kuwa dhamira yake ni kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara, afya, elimu na upatikanaji wa maji safi ili kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi wote wa Jimbo la Ileje bila ubaguzi.
Katika mkutano huo , Mhandisi Kasekenya amemnadi mgombea urais wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na kuwaomba wananchi kumpa kura ili aendelee kuongoza nchi kwa miaka mingine mitano ijayo huku akisisitiza kuwa Dkt. Samia amefanya mambo makubwa katika kipindi chake cha uongozi, ikiwemo kuboresha barabara katika Jimbo la Ileje na miradi mingine ya maendeleo iliyosaidia kuinua hali ya maisha ya wananchi huku akiwaomba wakazi wa Ileje kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kuhakikisha ushindi wa CCM.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania