[ad_1]

gfv

Chanzo cha picha, KCNA

Maelezo ya picha, Kim Ju Ae (anayeonekana hapa 2023) amekuwa mtu wa kawaida katika gwaride la kijeshi huko Korea Kaskazini katika miaka michache iliyopita.

Kuwasili kwa Kim Jong Un nchini China katika mkutano na nchi hiyo kumebeba vichwa vya habari.

Lakini msichana aliyevalia nadhifu aliyesimama nyuma yake alipokuwa akitoka kwenye treni yake ya kivita ndiye aliyevutia zaidi: Kim Ju Ae, bintiye kiongozi wa Korea Kaskazini.

Kulingana na shirika la kijasusi la Korea Kusini, Ju Ae ndiye anayetarajiwa kuwa mrithi wa babake.

Ju Ae, anaaminika kuwa mtoto wa pili wa Kim Jong Un na mke wake, Ri Sol-Ju, wakiwa na watoto watatu. Hata hivyo Kim ni msiri sana kuhusu familia yake, alimtambulisha mkewe kwa umma baada ya muda mrefu kupita tangu kuoana.

[ad_2]

Source link

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *