Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa wito wa mshikamano wa kitaifa, akisisitiza umuhimu wa kudumisha amani, umoja na utulivu baada ya kuapishwa kwa muhula mpya wa miaka mitano. Katika hotuba yake jana mjini Dodoma, Samia alieleza kuwa Tanzania inahitaji kujenga maridhiano ya kitaifa na kuendeleza utamaduni wa demokrasia unaozingatia haki, usawa na ushirikishwaji wa wananchi wote.