Timu ya Al-Hilal SC Omdurman yaSudan, ambayo tayari imefuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika imetangaza kuwa itakuwa inachezea mechi zake za nyumbani katika Uwanja wa taifa wa  Rwanda wa Amahoro, uwanja ambao mara nyingi ni gharama kubwa kwa timu nyingi za Rwanda.

Mwenyekiti wa Al Hilal SC, Yasir Hassan Ibrahimamelishukuru shirikisho la soka nchini Rwanda, FERWAFA kwa kuzipa timu hizo fursa ya kushiriki ligi ya Rwanda.Alikuwa na haya yakueleza.

 “Tunashukuru kwa mapokezi mazuri na kwa kukubali ombi letu la kushiriki Ligi Kuu ya Rwanda. Sisi tupo kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League), na tunaamini ligi hii itatusaidia katika maandalizi yetu.”

Kocha timu ya APR ya Rwanda,  Talib Abderrahim kuhusu ujio wa timu hizi za Sudan, amesema kwamba ni muhimu sana kwa ligi ya Rwanda.

“Timu hizi nazifahamu vizuri. Wachezaji wengi wa timu hizo wako katika kiwango cha juu, unapocheza na timu yenye wachezaji bora,  unapata nguvu na motisha zaidi” amesema Talib.

Soka la Rwanda litanufaika sana. Wachezaji wetu watainua viwango vyao kwa kukutana na timu zenye viwangu bora. Namshukuru mtu aliyefanikisha ujio wa timu hizo.”

Al-Merrikh nayo itawasili Rwanda

Inatarajiwa kwamba timu nyingine kutoka Sudan, Al-Merrikh, itawasili Rwanda kesho kutwa  Jumatano. Timu hizi zimeyakimbia machafuko yanayoendelea  nchini kwao Sudan.

Amahoro
Uwanja wa taifa nchini Rwanda wa AmahoroPicha: GUILLEM SARTORIO/AFP/Getty Images

Tukiwa bado nchini , kwa muda mrefu, uamuzi  wa baadhi ya marefa umekuwa ukichafua Ligi Kuu ya Rwanda na kusababisha kusimamishwa kwa waamuzi  huku uongozi wa Shirikisho la Soka laRwanda ukichukua hatua.

Matatizo hayo, yakiwemo tuhuma za upangaji wa matokeo na makosa makubwa yanayobadilisha matokeo ya michezo, yameibua lawama kutoka kwa mashabiki na maafisa wa soka.

Kulingana na Shirikisho la soka la Rwanda,FERWAFA lina mpango wa kutumia teknolojia ya VAR kwa siku za hivi karibuni, kuwapa mafunzo waamuzi wa ndani kuhusu jinsi ya kutumia teknolojia ya VAR, kutaboresha taaluma yao. 

Hii haitanufaisha tu ligi ya ndani bali pia itawaandaa waamuzi wa Rwanda kwa majukumu ya kimataifa yajayo.

Christopher Karenzi, DW Kigali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *