Wizara ya Mambo ya Nje ya China imetangaza kuwa, Beijing inaunga mkono haki ya Iran ya kutumia nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani.

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema hayo katika taarifa yake siku ya Jumatano baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo kufanya mazungumzo kwa njia ya simu na mwenzake wa Iran.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema kuwa, Wang Yi katika mazungumzo ya simu na mwenzake wa Iran, Seyyed Abbas Araghchi, alisema kuwa kushindwa kutatua suala la nyuklia la Iran si kwa maslahi ya jamii ya kimataifa. Taarifa hiyo iliongeza: Wang Yi pia alisisitiza uungaji mkono wa China kwa “haki ya Iran ya kutumia nishati ya nyuklia kwa amani.” Waziri wa Mambo ya Nje wa China alisema: “Beijing inatumai kuwa pande zote zitadumisha mazungumzo na mawasiliano ili kurudisha suala la nyuklia la Iran kwenye mkondo wa mazungumzo.”

Kwa upande wake Sayyid Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, sambamba na kuthamini msimamo wa China wa kuwajibika na wa kimsingi katika kutangaza mchakato unaoitwa “snapback” katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa ni kinyume cha sheria, alijadili na kubadilishana mawazo na mwenzake wa China katika mazungumzo hayo ya simu

kuhusu hali ya hivi karibuni ya uhusiano wa pande mbili na matukio ya kikanda na kimataifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *